Utangulizi Mbalawala Women Organization (MWO) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) lililopo katika wilaya ya Mbinga. Makao makuu ya MWO yapo katika kijiji cha Ruanda, eneo la center D.

Mbalawala Women Organization ni matokeo ya juhudi za Tancoal Energy Limited katika kuisaidia jamii inayozunguka mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka. MWO imeundwa na vijiji vya Ruanda na Ntunduwaro, Tancoal Energy Limited na kikundi cha Umoja wa Wanawake Mbalawala (Mbalawala Women Association).

  • ¬†Ruanda na Ntunduwaro: ni vijiji jirani vinavyozunguka mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka
  • ¬†Umoja wa Wanawake Mbalawala: ni kikundi cha wanawake walioungana kutoka vijiji vya Ruanda na Ntunduwaro
  • TANCOAL: ni mwekezaji wa mgodi wa makaa ya mawe Ngaka . Maana ya neno Mbalawala Neno Mbalawala limetokana na jina la mto uliopo karibu na eneo la mgodi mmojawapo wa machimbo ya Ngaka.