Lengo kuu la MWO

Kuwawezesha wanawake kupata fursa ya ajira katika miradi mbalimbali kupitia uwepo wa mgodi wa makaa ya mawe. Ziada itakayopatikana kutokana na uzalishaji katika miradi hiyo itatumika katika huduma za jamii kama hospitali na shule katika vijiji husika.

  • Malengo
  1.  Kuwawezesha wanawake wanaoishi karibu na mgodi wa makaa ya mawe kufanya shughuli za uzalishaji mali na kutoa huduma katika kambi ya mgodi, na ziada inayopatikana kutumika katika maendeleo ya vijiji vya Ruanda na Ntunduwaro
  2. Kuwapatia uwezo wanawake waweze kushiriki kutoa maamuzi katika jamii • Kuboresha maisha ya jamii kupitia matumizi bora ya maliasili zilizopo
  3. Kutunza mazingira kwa kutengeneza na kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala itokanayo na makaa ya mawe.
  4. Kushirikiana na jamii kuboresha elimu, afya na usafi wa mazingira