Programu ya shule

Programu ya shule inahusu uhamasishaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari katika vijiji hivi. Lengo ni kuwahamasisha wanafunzi wajifunze kwa bidii na pia kuwatia hamasa ya kusomea masomo yanayohusu masuala ya mgodi hapo baadae wafikapo elimu ya juu – ili wawe wataalam wa baadae katika mgodi.

Uhamasishaji unafanyika kupitia kutoa motisha mbalimbali kwa wanaofanya vizuri katika masomo.Mfano tayari wanafunzi waliopata alama za juu katika shule za msingi na sekondari wamepatiwa fulana na wameshaanza ziara za kimafunzo katika mgodi. Motisha nyingine inayotarajiwa kutolewa ni pamoja na kupatiwa fulana, daftari, vitabu, unifomu. Pia kuchangiwa ada hasa kwa wale wanaoishi katika mazingira magumu (watakaopata alama za juu darasani).