Lengo:

  • Kutumia vizuri mali asili ya udongo kwa kutengeneza vyombo vya nyumbani
  • Kuongeza ujuzi wa ufinyanzi • Kutumia maliasili ya udongo kuongeza kipato Ufinyanzi unaofanyika ni pamoja na utengenezaji wa vyungu vya kupikia, vyungu vya maji na vya maua pamoja na majiko ya kupikia yanayotokana na udongo. Kwa sasa ufinyanzi unafanyika kwa kutumia mikono. Tayari MWO imepokea mashine ya kutengenezea vyungu kupitia Tancoal Energy Limited. Pindi jengo la vyungu litakapojengwa mashine hiyo itafungwa na kuanza kutumika. Wanawake 4 wameajiriwa katika mradi wa vyungu.

Tayari MWO imepokea mashine ya kutengeneza vyungu kwa uhisani wa ubalozi wa Australia kupitia Tancoal Energy Limited.