Utengenezaji wa vitofali vya kupikia vya makaa ya mawe

Lengo:

  • Kutunza mazingira – kupunguza ukataji miti kwa kutengeneza na kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala ya vitofali vya kupikia vya makaa ya mawe Mradi huu upo katika hatua ya awali. Tayari mashine imeshanunuliwa kupitia Tancoal Energy Limited.

Majaribio ya utengenezaji yameshafanyika, matokeo yameonyesha mafanikio- vitofali vyenye ubora vilitengenezwa kwa kutumia mavumbi ya makaa na malighafi zinazopatikana katika maeneo haya.

Mpango uliopo ni kujenga jengo litakalotumika katika uzalishaji wa vitofali hivyo kabla ya Novemba 2013. Kitengo hiki kinatarajiwa kuanza na wafanyakazi watatu.

Tayari mashine imeshanunuliwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Australia kupitia Tancoal Energy Limited.