Mbalawala Women Organization imekuwa ikishirikiana na jamii kwa:

a) Kusaidia shughuli za vikundi vidogo vidogo katika miradi ya ki-uchumi. Tayari vikundi viwili vimefaidika katika miradi ya kuku na kilimo cha uyoga katika vijiji hivi.

b) Kufanya kazi za usafi wa mazingira kwa kujitolea katika hospitali , zahanati na katika taasisi za umma katika vijiji vya Ruanda na Ntunduwaro.

Ajira

Hadi wezi Julai 2013, MWO imeajiri jumla ya wafanyakazi 25, kati ya hao wanawake ni 23 na wanaume ni 2. Wafanyakazi wote wamejiunga na NSSF Ajira kwa wanawake wa vijiji husika itaendelea kutolewa kadri miradi itakavyopanuka.

Fursa nyingine katika jamii

Wananchi katika vijiji hivi wanapata soko kwa kuuza mazao ya vyakula na mifugo katika kambi ya mgodi.